Z ANTO AJA KIVINGINE

 

  • Awachana wasanii wadogo wanaotoka kimapenzi na watu wazima na wale wanaoringa kisa kuwa na majina makubwa

 

Msanii aliyewahi kutamba na vibao kadhaa ikiwemo ‘Binti Kiziwi’ ambayo ilimpa umaarufu pamoja na ‘Mpenzi Jini’ amerudi katika game kwa kuachia video yake mpya aliyoipa jina la ‘Kacheze Unapochezaga’ chini ya label yake mpya ya ‘Lavi Davi Entertaiment’ iliyoandaliwa na director Msafiri wa Kwetu Studio.

 

 

Katika Video yake hiyo Z Anto amekuja kivingine tofauti na tulivyokuwa tumezoea kuziona nyimba zake zilizopita na katika baadhi ya mistari yake ameonekana akiwasema baadhi ya wasanii ambao huwa wanalewa sifa na kusahau walipotoka.

Watu wengi wanajiuliza je ataweza kukimbiza tena kama alivyowahi kukimbiza hapo awali nah ii ni kutokana na game ya sasa hivi kuwa tough na kila mtu anapambana ili aweze kuwa juu na pia muziki wa sasa hivi umekuwa na ushindani mkubwa wasanii wanafanya muziki kwa ajili ya biashara zaidi na wapo wengi tofauti na ilivyokuwa awali wasanii walipokuwa wachache.

 

Please follow and like us:

Comments

comments