WAKURUGENZI WA HALMASHAURI 30 MATATANI

• Watakiwa kutoa maelezo kwa kushindwa kuwawezesha maofisa maendeleo jamii kufika katika mkutano wa 12 wa kujadili maendeleo ya jamii

Katika mkutano huo wa kikazi wa maofisa hao, halmashauri zilizopeleka wajumbe ni 30 tu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Selemani Jafo alisema kitendo cha wakurugenzi hao kinazuia nia njema ya Serikali ya kusukuma maendeleo kwa wananchi wake.
Alisema maofisa hao wana kazi nyingi za maendeleo ya wananchi na kutowawezesha katika mkutano ni kuwanyima maarifa mapya ya kazi na hasa kubadilishana uzoefu kati yao. Alisema serikali inawategemea maofisa hao kufanikisha miradi ya maendeleo hasa ile ya elimu na ufahamu kuzuia mitafaruku maeneo yao na kuhamasisha maendeleo ya jamii.
“Wananchi wana matarajio makubwa na serikali na mabadiliko hayawezi kuja bila kuwa na mabadiliko katika utendaji kazi,” alisema. Alisema kutokana na wajibu wao, serikali sasa inapiga marufuku maofisa hao kusimamia miradi ya Tasaf na Ukimwi pekee bali waandae mikakati ya kuwawezesha wananchi kutambua fursa na kutekeleza miradi ya maendeleo yao.
Waziri Jafo aliwataka maofisa maendeleo ya jamii kufanya kazi ya kupiga vita maovu katika jamii ikiwamo mauaji ya vikongwe na albino. Ofisa Maendeleo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam Mwajuma Magwizu kwa niaba ya wenzake alisema watatekeleza maagizo waliyopewa kwa ufasaha ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

Please follow and like us:

Comments

comments