VANESSA MDEE NA JUX KURUDIANA?

  • Ni baada ya kuonekana kuwa na ukaribu uliopitiliza wakiwa Fiesta.

 http://niaje.com/wp-content/uploads/2015/01/vee.jpg

 

Love birds waliowakuwa katika mahusiano ya kimahaba kabla ya shetani mkata kamba kupita, Vanessa Mdee aka Vee Money na Juma Jux ambao hivi karibuni walitangaza kuvunjika kwa mahusiano yao, wameonekana wakiwa na ukaribu wa hali ya juu na kupelekea watu kuhisi kuwa huenda watarudiana hivi karibuni.

Katika tamasha la Fiesta lililofanyika mkoani Iringa mrembo Vee Mapesa anayetamba na kibao chake cha “Kisela” aliibuka na kuimba wimbo unaokwenda kwa jina la “Juu”,ngoma aliyowahi kufanya na mpenzi wake wa zamani Jux ambaye nae kwa sasa anafanya poa sana katika gemu la muziki na kutamba na ngoma yake ambayo ni tru stori ya “Utaniua”.

Kitendo hicho cha wawili hao kimepelekea mashabiki wengi kufurahishwa nacho na wengi wakionekana kuwaombea waweze kurudisha mahusiano yao.

Please follow and like us:

Comments

comments