TUNDA AKANA KUTOKA KIMAPENZI NA MMBONGO FLEVA

• Adai huwa anamuweka katika mitandao ya kijamii kwa sababu ta ku-support kazi zake

Muuza nyago katika video za wasanii tofauti tofauti hapa Bongo, Tunda Sebastian ‘ Tunda’ amekana kuwa na ujauzito kama watu wengi wanavyodai.
Tunda amesema kuwa hana ujauzito wa msanii huyo kama watu wanavyosema na kuongeza kuwa huwa anamuweka katika mitandao ya kijamii hasa Instagram kwa sababu yak um-support kazi zake.
“ Ndio kwanza nasikia kwenu, siyo kweli na sina mimba yake, huwa namuweka Insta kumsapoti kikazi tu maana ni rafiki yangu sana lakini watu walivyoona hivyo wakaanza kuzusha maneno hayo kwamba ninatoka naye na nina mimba yake na kuhusu kunenepa, nimenenepa kwa sababu nimeridhika na maisha mazuri niliyo nayo” alisema Tunda.

Please follow and like us:

Comments

comments