SOUDY BROWN ATEMA CHECHE

• Ni baada ya mrembo mmoja kumlalamikia jamaa huyo kutumia lugha moja tu akiwa anagawa ubuyu

Mwandishi na mtangazaji machachari wa kipindi maarufu hapa town cha Shilawadu Soudy Brown ameibuka na kumwaga maneno heavy kwa mmoja wa shabiki wake.
Kupitia mtandao wa Instagram Soudy ametokwa na maneno hayo baada ya fan huyo kuandika kuwa,
“He! He! He! Soudy, kwahiyo pale ambapo ni matangazo ya biashara in London unaweka caption za kiingereza ili fans wako wa London waweze kukuelewa vizuri lakini ikiwa ni suala la umbeya basi unaweka caption za Kiswahili ili fans wako wa London wasikuelewe, sisi pia tunataka caption za kiingereza katika posts zako za gossip” ameandika fan huyo ambapo Soudy hakusita kuijibu kuwa,
“My dear, hukunilipia ada yangu ya shule, pili, kuandika ubuyu(umbeya) kwa kiingereza haunogi kwahiyo usinichoshe kuandika English, na tatu kiingereza huku kimekuja na Boti” ameandika Soudy.

Please follow and like us:

Comments

comments