SOUDY BROWN ATANGAZA KUACHA KAZI YA UMBEA

• Asema bado yupo Moshi anaperuzi lakini bado haamini kama kuna ndoa kati ya Uwoya na Janjaro


Presdent wa Shirika La Wambea Duniani (SHILAWADU), Soudy Brown ametangaza kuacha shughuli ya umbea iwapo atathibitisha kama ni kweli Dogo Janja na Irene Uwoya watakuwa ni kweli wamefunga ndoa.
Kupitia page yake ya Instagram Soudy amesema kuwa haamini kama ni kweli kuna ndoa kati ya wawili hao na kuongeza kuwa ikiwa ni kweli basi atavua mask yake na kuacha umbea lakini ni mapak aone bibi harusi na bwana harusi wakiwa kwenye sherehe yao.

“ Nipo Moshi naperuz naperuz lakini bado siamini kama kweli kuna ndoa kati hawa wapendanao…..mbona hamna picha ya pamoja kati ya Bi Harusi na Bwana Harusi wakiwa kwenye sherehe yao,,, Kingine bado Ndikumana hajatoa talaka, kwa hiyo Dogo Janja ameoaje mke wa mtu?…… Kama wameoana kweli na ukatoka ushahidi taslimu basi mimi nalivua mask, na kazi ya umbea naacha” ameandika Soudy Brown.

Please follow and like us:

Comments

comments