SONIA AFUNGUKA NA KUWATAJA WALIOCHANGIA KUHARIBU SOKO LA BONGO MOVIE

• Amesema kuwa ni producers na baadhi ya wasanii pia aomba serikali kuingilia kati suala hilo


Muigizaji mkongwe wa movie za kibongo Farida Sabu amabaye wengi humwita Sonia amefunguka issue kibao ikiwemo kuyumba kwa soko la filamu za kibongo kwa sasa.
Kupitia mahojiano yake na See The African Movie amewatupia lawama baadhi ya waigizaji mastaa ambao walifanya kazi ya uandaaji na usambazaji,
“hii tasnia imeangushwa kwa mabo mengi sana, tumekuwa tukiitupia sana serikali lawama, wakati tunaanza filamu zilikuwa zinawalipa sana producers na sio sisi waigizaji, kiukweli walitengeneza pesa nzuri sana kupitia sisi, amabpo sisi tulikuwa tunalipwa kidogo na ndipo wasanii wakubwa waliokuwa na uwezo kuamua kufanya kazi zao wenyewe” amesema Sonia.
Pia akiongea kuhusu uwezekano wa kuirudisha Bongo movie ya zamani Sonia amedai kuwa inawezekana pale ambapo wataanza kutegemeana na serikali sio kusimama msanii kama msanii kwani uwezo huo hawana.

Please follow and like us:

Comments

comments