REKODI YAVUNJWA KATIKA MLIMA MREFU AFRICA

• Ni baada ya raia wa Hispania kufanikiwa kuvunja rekodi yakuupanda mlima huo kwa baiskeli

Mpanda milima mashuhuri duniani kwa kutumia Baiskeli, Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli kwa siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito na wenzake wawili, Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema, aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika
Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa za Kilimanjaro, Arusha na Saadani inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio vya utalii katika Hifadhi zake 16. Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anaeleza hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.

Please follow and like us:

Comments

comments