Rekodi 4 zilizowekwa baada ya Bayern kuisambaratisha Arsenal

Kuna rekodi nyingi mbalimbali zimewekwa baada ya Arsenal kuchezea kipigo cha magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani kutoka kwa Bayern Munich kwenye hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya na kufanya jumla ya magoli 10-2 baada ya michezo miwili kukamilika.

Bayern ilitoa kichapo cha magoli 5-1 kwenye mechi ya kwanza ilipokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Alianz Arena, ikarudia tena matokeo kama hayo kwenye mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa ugenini Emirates, England.

Hizi ni rekodi nne kubwa ambazo zimewekwa baada ya Arsenal kufungwa jumla ya magoli 10-2 baada ya mechi mbili na kutupwa nje ya michuano ya Ulaya kwa aibu ya aina yake.

  • Aggregate ya 10-2 ni matokeo mabaya kwa soka la England kuwahi kutokea kwenye historia ya klabu bingwa Ulaya.
  • Ilikuwa ni kipigo kikubwa zaidi kwenye uwanja wa nyumbani wa Arsenal tangu November 1998 (ilipopoteza 5-0 dhidi ya Chelsea) kwenye mchezo wa kombe la ligi.
  • Arsenal inakuwa timu ya pili kuondoshwa kwenye michuano ya Champions League kwa idadi kubwa ya magoli. Mechi ilivyoweka rekodi ya magoli mengi ni Bayern Munich vs Sporting Lisbon (Bayern ilifuzu kwa kuichapa Sporting Lisbon magoli 12-1 mwaka 2009).
  • Barcelona ndio ndio timu iliyofunga magoli mengi zaidi kwenye Champions League dhidi ya timu moja (imefunga magoli 27 dhidi ya Celtic) ikifatiwa na Bayern ambayo imeshaifunga Arsenal magoli 26 hadi sasa kwenye mechi za Champions League tangu timu hizo zilipoanza kukutana.

Matokeo ya Arsenal kwenye hatua ya 16 bora tangu mwaka 2011 ambapo hawajafanikiwa kufuzu hatua inayofata kwa misimu saba hadi sasa.

2010-11 Barcelona 3-4
2011-12 Milan 3-4
2012-13 Bayern Munich 3-3 (Bayern win on away goals)
2013-14 Bayern Munich 1-3
2014-15 Monaco 3-3 (Monaco win on away goals)
2015-16 Barcelona 1-5
2016-17 Bayern Munich 2-10
Please follow and like us:

Comments

comments