Mengi afunguka haya kuhusu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuvamia Clouds media

Kulia ni mkurugenzi wa IPP Media Reginald Mengi (kushoto) ni Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mh Nape Nnauye, akiwa pembeni na C.E.O wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, katikati ni mkurugenzi wa Habari maelezo Hassan Abbas.

Sakata la kuvamiwa kwa kituo cha Radio cha Clouds FM ndio habari ya jiji kwa sasa. Kufuatia tukio la kipekee ambalo halikuwahi kujitokeza, kwenye media hiyo,  tukio hili limekuwa na uzito kiasi cha kuzua mijadala mbalimbali ya sinto fahamu kutoka kwa Watanzania.

Kwa uzito wa tukio hilo baadhi ya viongozi wa serikali na wamiliki wa vyombo vya habari wamejitokeza na kupinga kilichofanywa na mkuu wa mkoa huyo.

Akiongelea suala hilo katika ofisi za Clouds Media mkurugenzi wa IPP Media alisema kuwa “Mimi nina imani kwamba tuna Raisi anayetupenda sana na tuna waziri anayetupenda sana . lakini mapenzi hayo lazima yaonyeshwe kwa vitendo.

Jambo lililofanyika ni la hatari sana lazima tujiulize mtu huyu (Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam) anapata wapi ujasiri huu? kama alikuwa na bunduki hapa anaweza kwenda nazo popote na pengine kuna siku atazitumia”. # Reginald Mengi.”

Please follow and like us:

Comments

comments