RAYVANNY AMNYAKUA KIBABE PRODUCER RASHDONI

• Utata ulikuja baada ya Producer Rashdoni kusepa Kiri Records na kwenda Surprise Rocords inayomilikiwa na Rayvann


Producer Rashdoni


Producer maarufu aliyekuwa Kiri Records, Rashdoni amedaiwa kuondoka kimya kimya katika studio aliyokuwa akifanyia kazi hapo awali na kuhamia katika studio za msanii kutoka katika label ya WCB Rayvanny iitwayo ‘Surprise Music Studio’.
Producer anayeshikilia mikoba ya Rashdoni kwa sasa Beya amesema kuwa Rashdoni aliondoka bila kuaga na walikuja kusikia baadae kuwa amehamia katika studio za Rayvanny.
“ Mimi ndio nilikuwa msaidizi wa Rashdoni, Meneja yupo, Bosi yupo lakini aliondoka bila kuaga yaani ilifikia kipindi alikuwa haji kabisa studio au akija ana dash yaani leo anakuja kesho haji, tunakuja kusikia wakati Diamond anafanya interview ya wimbo wake wa fire aliofanya na Tiwa Savage, tukasikia anasema kwamba Rashdoni ndio official producer wa Rayvanny, kwa hiyo sis hatukuwa na la kusema”. Amesema Beya.

Producer Beya

Rashdoni naye alikana tuhuma za kuwa aliondoka bila kuaga na kudai kuwa mkataba wake katika studio hizo ulikuwa umeisha na bosi wake alikuwa analijua hilo.
“ Ukisema kuwa niliondoka bila kuaga unakuwa unakosea, mimi sijawahi kupotea ghafla na bosi aliniuliza nina mpango gani kwa sababu makataba wangu ulikuwa unaisha, nikamwambia bosi tulia nitakuambia nina mpango gani kwa hiyo ofcourse sikumkimbia mtu” alisema Rashdoni

Please follow and like us:

Comments

comments