RAMMY GALIS: WABONGO WANAJUA KUJIONGEZA

• Aikana skendo ya kutoka kimapenzi na msanii mwenzake Nikole

Msanii aliyeitendea haki filamu ya Chausiku aliyocheza na Shamsa Ford, Rammy Galis amekana kutoka kimapenzi na msanii mwenzake Naomi Salakikya ‘Nikole’ na kudai kuwa ni uvumi tu ambao watu wameamua kuusambaza.
Rammy amesema kuwa maneno hayo yalianza kuzungumzwa kutokana na ukaribu waliokuwa nao wakati wanazindua movie ya ‘Red Flag’ zilizopita ambayo walishirikishwa na wasanii kutoka Nigeria.
“Acha watu waongee wanavyojisikia, ukweli ni kwamba Nikole ni mtu wangu wa karibu, kama rafiki yangu, kama dada yangu si mambo ya mapenzi kama watu wanavyodhani, si unajua Wabongo kwa kujiongeza,”alisema Galis.

Please follow and like us:

Comments

comments