RAIS TRUMP AUKANA UZEE

• Ni baada ya Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kumuita mzee na mchochezi


Wakati vita vya maneno vikiendelea kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un inaonekana Trump kuguswa zaidi na kauli zilizotolewa na serikali ya Korea Kaskazini kwa kumuita kuwa ‘mzee na mchochezi wa vita’ kitu ambacho kimemfanya aweke wazi hisia zake kuwa angefurahi siku moja kuona wanakaa meza moja na Kim.

Wizara ya mashauriano ya nchi za kigeni nchini Korea Kaskazini jana ilimuita Trump kuwa ‘mchochezi wa vita na mzee’ na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya kutengeneza silaha za nyuklia.
Kauli ambayo Rais Donald Trump alishindwa kujizuia kuijibu kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee wakati yeye hata siku moja haijawahi kutokea kumkebehi kuwa mfupi na mnene.

“Kwanini Rais Kim Jong-un ananitukana kuwa mimi ni mzee wakati mimi hata siku moja sijawahi kumuita yeye mfupi na mnene? Sawa najaribu kila niwezalo kuwa rafiki yake najua ipo siku tutakuwa marafiki.“ameandika Rais Donald Trump.

Please follow and like us:

Comments

comments