PIGO KWA MREMBO IRENE UWOYA

• Ni baada ya kuondokewa na aliyekuwa mume wake wa zamani Ndikumana

Mume wa zamani wa mrembo anayefanya poa katika Bongo movies Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amabye pia alikuwa ni kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda amefariki dunia.
Uongozi wa timu hiyo umesema jana Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya lakini mwili wake umekutwa nyumbani kwake mjini Kigali akiwa amefariki dunia.
Mpaka sasa bado haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajafanya ajali. Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram marehemu Ndikumana alitupia ujumbe wa shukrani kwa mama yake juu ya kuchagua mwanamke atakayemfaa kuishi naye.

Please follow and like us:

Comments

comments