OMOG: HAKUNA KOCHA AMBAYE YUPO MAHALI SALAMA DUNIANI

 

http://www.thecitizen.co.tz/image/view/-/3884414/medRes/1611559/-/x09h4f/-/pic+simba+vs+azam.jpg         Kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema hakuna kocha wa soka ambaye yupo mahali salama duniani ndiyo maana kila siku timu zinafanya mazoezi ili kurekebisha makosa yanayojitokeza na kuongeza uwezo wa wachezaji.

Akizungumzia suala hilo Omog alisema kuwa matokeo ya mpira huwa hayafurahishi kwa asilimia 100 na hiyo hupelekea makocha kufukuzwa na kuajiriwa kila mara katika klabu mbalimbali ndani nan je ya nchi.

“Hakuna kocha ambaye yupo mahali salama, ndiyo sababu kila siku timu zinafanya mazoezi ili kurekebesha makosa yanayojitokeza na pia kuongeza uwezo wa wachezaji, na nina matumaini mambo mazuri yanaweza kukuondoa au kukubakisha kwenye klabu”alisema Omog.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa mechi zote za ligi kuu Tanzania Bara zina ushindani kwa sababu wachezaji wameanza kuelewa na kuthamini umuhimu wa kazi wanayoifanya kutokana na kujifunza kwa yale yanayotokea kwa wachezaji wa klabu za Ulaya.

Please follow and like us:

Comments

comments