OMARION AKIRI KULIPENDA BARA LA AFRIKA

• Asema Marekani hawaonyeshwi mazuri ya Afrika bali wanaonyeshwa upande wa maskini tu

Msanii kutoka Marekani ambaye amefanya show usiku wa kuamkia leo hapa Bongo, Omarion amekiri kuwa anaipenda Tanzaia na Bara la Afrika kwa ujumla kutokana na uzuri wa asili ambao upo katika nchi nyingi katika bara la Afrika.
Omarion amesemakuwa sio mara yake ya kwanza kuja Tanzania na kusema kuwa Tanzani na Afrika kwa ujumla ni sehemu nzuri ambayo wamarekani wengi weusi hawalijui hilo.
“ Johanesburg, Durban na Tanzania ni kuzuri na ni pazuri kutembelea na kula raha, Marekani hawaonyeshwi mazuri ya Afrika wanaonyeshwa tu upande wa masikini…. Kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Marekani waliopata nafasi ya kufanya kazi na wasanii kama Diamond na wasanii wengine wa Afrika ni upendo” amesema Omarion.

Please follow and like us:

Comments

comments