NUH AKANA KUIMBA NA ALIYEMCHUKULIA MKE

• Hii ni baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anafahamiana na mwanaume huyo na wameshafanya wimbo pamoja


Baada ya habari kusambaa katika mitandao ya kijamii kuwa mawanaume aliyemuoa aliyekuwa mke wa Nuh Mziwanda kwamba aliwahi kufanya naye kazi na ndiye aliyemtoa kijijini kwa Iringa.
Nuh amekana taarifa hizo na kudai kuwa hamfahamu mwanaume huyo kama watu wanavyodai kuwa alimtoa Iringa na kuja kukaa naye ambapo ndipo alipofahamiana na mke wake.
“ Simfahamu kabisa huyo mwanaume zaidi ya kumuona kwenye picha, nawaomba mashabiki wangu wasinihusishe kabisa na hao watu maana kama ni Nawal yupo na maisha yake na mimi nipo na maisha yangu, nipo kikazi zaidi kwani kwa sasa ninatembea mikoa mbalimbali kufanya show wala sina habari na mtu” alisema Nuh Mziwanda

Please follow and like us:

Comments

comments