NIKIMCHOKA DIAMOND NAMUACHA SIHITAJI PESA ZAKE

 

  • Adai kuwa yeye ni tajiri hategeme pesa za Diamond hivyo hahitaji pesa za mwanaume yeyote

  

Mfanyabiashara na Mzazi mwenza wa Mwanamuziki Diamond, Zari the Bosslady amekuja tena na nyingine kali akidai kuwa yeye ni mwanamke tajiri na pesa zake hivyo hahitaji pesa za mwanaume yoyote hasa Diamond kwani tayari anajiweza na endapo siku ikifika akichoshwa na matendo ya Diamond basi atamuacha na hatahitaji hata senti yake kwani yeye mwenyewe ni boss.

Tangu mpenzi wake Diamond alipom-cheat na kuzaa na Hamisa, Zari ametumia muda wake mwingi kugombana na Hamisa na kumrushia vijembe mtandaoni jambo ambalo watu wengi wameshangazwa kuwa ni kwa nini agombane na Hamisa wakati Diamnd ndio aliyemsaliti lakini Zari alijibu kuwa hana muda na mtu yeye anaongea anachoongea kikikuuma basi ujue lako hilo.

Pia Zari alimrushia dongo Hamisa kwa kitendo chake cha kuomba pesa ya matunzo ya mtoto na kudai kuwa hata siku moja hatakaaa aje ampeleke mahakamani mwanaume kwa sababu amekataa kulea mtoto wake bali ataondoka na kwenda kulea mtoto wake bila kuhitaji huduma kutoka kwa mwanaume kwa sababu ana uwezo huo.

Zari aliongelea mambo ya pesa ya malezi ya mtoto kwa sababu Hamisa kampeleka mahakamani Diamond kwa sababu amekataaa kumlea mwanae aliyezaa naye anayejulikana kama Dylan.

Please follow and like us:

Comments

comments