NDOA YA SHILOLE, KIINGILIO MIGUU YAKO

 

  • Amesema kuwa ndoa yake hatafanya siri na haitakuwa na kiingilio

 

Msanii asiyeishiwa vituko, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa yake mwezi December mwaka huu na mpenzi wake Ashirafu Uchebe na haitakuwa na kiingilio kama ilivyozoeleka kwa sherehe nyingine.

Shilole amesema kuwa ndoa yake itafanyika sehemu ya wazi ambayo kila mtu anaweza kufika na kuongeza kwa anamshukuru Mungu mpenzi wake ameshalipa mahari kubwa nyumbani kwao, na kilichbaki ni ndoa tu na haitakuwa na watu maalum kama ilivyozoeleka.

“ Ndoa yangu sitafanya siri kama wanavyofanya watu wengine, nitafanya sehemu ya wazi kabisa na wala haitakuwa na kiingilio hata kidogo, maana napenda watu wote waone na washuhudie kinachoendelea” alisema Shilole.

Please follow and like us:

Comments

comments