MWACHENI DIAMOND NA VIEWS ZAKE

kuwa die hard fan wa msanii kuna maana nyingi sana inawezekana unapenda style ya muziki wake,mavazi,maisha yake binafsi au hata muonekano wake.
kwa kipindi kisichozidi miaka minne Tanzania kumekua na uhasimu baina ya wasanii wawili Diamond Platnumz na Ali Kiba ,uhasimu huu kwa nje unaonekana ni vita kali zaidi za mashabiki wa wasanii hawa.
Si vibaya kuwa mnazi wa msanii yoyote yule ila ubaya ni pale inapotumika mguvu kubwa kupumbaza wengine ili kufanikisha azma binafsi ya kifikra na nadharia.
Siku ya Alhamisi Diamond Platnumz alitoa wimbo unaoitwa Hallelujah ambapo katika wimbo huo Diamond amelishirikisha kundi kongwe la muziki wa reggae Duniani “Morgan Heritage” wimbo huo pamoja na Video vilipasua mitandao ya kijamii ndani ya masaa machache sana, na kuanza kuingia katika mzunguko wa kusikilizwa ndani ya muda mfupi , ndani ya masaa 15 tu wimbo huu ulitazamwa mara millioni moja. Kimahesabu millioni moja ukigawanya mara 15 utagundua wimbo huu ulitazamwa kwa wastani wa Mara zaidi ya elfu 66 kila baada ya Saa moja ,Mara 1,100 kila baada ya dakika moja na Mara 18 kila baada ya sekunde Moja

 

Takwimu za video ya wimbo huu zimeanza kuibua mjadala ambao ukiutazama kwa umakini utagundua hauna mantiki sana ila ni kikundi cha watu kinachotaka kuwapumbaza mashabiki wa muziki Tanzania tena wa pande zote wenye team na walioko katikati. Wapo wanaotaka kutuambia kuwa namba za watazamaji wa video ya wimbo huu zimenunuliwa yani sio kweli kwamba msanii wa Tanzania anaweza kupata viewers milioni moja ndani ya masaa 15, ukitafakari kwa ushawishi alionao Diamond katika Mtandao wa Instagram pekee utagundua kuwa ana wafuasi zaidi ya Millioni 4, kuwa na wafuasi zaidi ya Millioni 4 si kitu kidogo kwanza Africa Mashariki na kati hakuna msanii mwenye ushawishi mkubwa mitandaoni kama Diamond fahamu hilo chukua nusu tu ya millioni 4 ambayo ni million 2 wangeweza kuifanya video hiyo ikatazamwa mara mbili ya ilivyotazamwa , hivyo ushawishi wa Diamond Mitandaoni unatosha kabisa kumfanya aendelee kuweka na kuvunja record za kutazamwa katika mtandao wa YouTube. Pia tukumbuke collabo hii Diamond hajafanya na wasanii wa kawaida collabo hii Diamond amefanya na Kundi la Morgan Heritage lenye mashabiki kila kona duniani na pia ni kundi kongwe kama hufahamu albam ya kwanza ya Morgan Heritage ‘miracles’ ilitoka mwaka 1994 miaka 23 iliyopita na wamedumu mpaka leo hivyo wana mashabiki wa vizazi tofauti tofauti katika miongo zaidi ya miwili , Kubwa zaidi miaka miwili iliyopita Morgan Heritage walishinda Tuzo kubwa zaidi na ya kuheshimika duniani Tuzo ya Grammy kupitia Albam yao ‘Strictly Roots’ hivyo profile yao ni kubwa sana na hata credibility yao si ya ‘kumumunyamumunya’ hivyo katika hao watu milioni moja walioitazama kwa masaa 15 sio kwamba wote ni mashabiki wa Diamond pekee. Penye sifa ni vyema kutoa sifa tu tatizo ni kwamba kumeibuka watu wengi sana wanaojiita wachambuzi wa muziki ambao wao hawafanyi uchambuzi ila ni wazuri katika kuelezea mambo wanayopenda, na baadhi ya watangazaji ni watangazaji sio kwa sababu wana taaluma ya habari bali ni sababu tu wana sauti nzuri, muonekano na jina mjini watu hawa hucheza sana na akili za watanzania na kuwapumbaza.

Hakuna wakati mzuri wa wasanii wa Tanzania kutumia fursa zilizopo ndani ya Tamaduni mpya ya watanzania kutumia sana mitandao ya kijamii kama wakati huu.Pima uzito wa msanii kama Aslay katika Tasnia ya muziki Tanzania na ufahamu kuwa si Kenya wala Uganda hawana msanii mwenye ufuasi mkubwa instagram kama Aslay tu, ndio maana Aslay ametazamwa zaidi ya mara millioni 9 YouTube katika kipindi cha miezi mitano tu. ni ukweli usiopingika kuwa watanzania wa rika zote wamekua watumiaji wa mitandao ya kijamii hivyo kinachoonekana ni ushiriki wao na sio miujiza, kama tumeweza kuwapa wasanii wetu tuzo za kkimataifa kwa kupitia kura za mitandaoni na tukawazidi mpaka wanaigeria ambao kwa idadi ya watu wametuzidi sana kwanini tujishangaze kwa Diamond kupata views nyingi?

Please follow and like us:

Comments

comments