Msanii Ciara mwenye ujauzito apata ajali ya Gari!!

Nyota wa RnB Ciara amepata ajali ya gari usiku wa kuamkia 11 March 2017. Ciara ambaye anaujauzito wa mtoto wake wa pili amepata ajali mjini L.A.

Ciara alikuwa akiendesha Mercedes SUV nyeupe na alikuwa akipiga kona kwa kupande wa kushoto na ndipo alipogongwa na gari nyingine aina ya Volvo SUV.

Gari hilo liligonga upande wa abiria na kumuumiza kifua Ciara ila taarifa kwa sasa zinasema Mama na mtoto wote wako salama

Mume wa Ciara ‘Russell Wilson‘ aliandika twitter  “Momma Wilson & Baby Wilson are feeling great! God is good!

Please follow and like us:

Comments

comments