MR NICE AMPA SOMO ASLAY

• Amesema kuwa wanamuziki hawatambi muda wote na kwa style yake anaweza akakosa cha kutoa hapo baadae

Mkongwe aliyewahi kutamba na nyimba kadhaa pamoja na style yake ya kucheza ya (TAKEU), Tanzania, Kenya na Uganda, Mr. Nice ameamua kumpa somo msanii anayetamba kwa sasa hapa Bongo, Aslay kutokana na tabia yake ya kutoa nyimbo mfululizo.

Mr.Nice amesema kuwa Aslay anachokifanya ni kuua muziki wake kwa sababu itafika muda hapo baadae atakosa cha kutoa na anachokifanya kwa sasa ni kuwachanganya mashabiki wake kwa sababu hawajui wasikilize wimbo upi.

“ Kwa namna Aslay anavyofanya muziki wake ni yeye mwenyewe anaua nyimbo zake, ndani ya mwezi mmoja huwapi mashabiki nafasi ya kusikiliza wimbo vizuri, unapotoa wimbo mpya kila mwezi unawachanganya akili na kufanya warukie huo mpya na kuutupa uliotangulia, kwa hiyo hilo aliangalie lakini pia aangalie kuhusu anguko lake” amesema Mr.Nice.

Please follow and like us:

Comments

comments