MR CHUZ WASANII ACHEKI KIKI

 

  • Ni baada ya kusema kiki hazina mpango hivyo waache kwani zinawabomoa na kuua soko la filamu

     Mwigizaji mkongwe katika industry ya bongo movie ,Tuesday Kihangala aka Mr chuz ametema cheche kwa wasanii wenzake kuacha mambo ya kiki kwani hazina maana bali zinawabomoa na kuzidi kuua tasnia ya filamu

Mkongwe huyo amedai kuwa wasanii wanatakiwa kuelewa kwamba kik bila kufanya kazi ni bure kwani mashabiki wanachotaka ni kuona kazi zao bora na siyo kiki au skendo zisizokuwa na kichwa wala miguu

‘jamani wasanii wenzangu pigeni kazi,achaneni na kiki kwani siyo mpango ,niko huku lushoto kwa miezi kadhaa sasa nafanya kazi ya tamthiliya na nimeshamaliza Closed Chapter sasa naanza nyingine mpya naamini kila msanii angekuwa kama mimi,tasnia ya filamu ingerudi kwenye ubora wake kama zamani “amesema chuz

 

 

 

 

 

Please follow and like us:

Comments

comments