MIMI MARS SIJAKOPI MELODY YA VANESSA

 

  • Ni kutokana na madai ya melody ya dede kuwa amecopy kwenye wimbo wa Vanessa wa duasi

 

Msanii wa muziki Bongo, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sitamani’, Mimi Mars amefunguka ishu ya kukopi melody kutoka Vanessa Mdee.

Mimi amedai kuwa si kweli ngoma yake ‘Dedee’ amechukua melody kutoka kwenye ngoma ya Vanessa na Legendury Beatz  ‘Duasi’ ila ni watu kusindwa kutofautisha

“Sijui labda zinafanana lakini nahisi kila mmoja ana njia yake, unaweza kukuta kitu kidogo tu ukasema hii kama ya wimbo ule lakini hiyo ipo hata kwenye muziki wa nje” Amesema Mimi Mars.

Please follow and like us:

Comments

comments