MCHEZAJI AMSHINDILIA KOCHA WAKE NGUMI

 

  • Hii ni baada ya kocha wake kumtoa nje na kumalaumu kuwa licha ua kufunga lakini bado alimtoa nje

 

 

Kiungo wa timu daraja la kwanza nchini Scotland ya Iametoa kali baada ya kumshambulia kocha wake wakati wakiwa katika mechi.

Polworth (22) alifanya kitendo hicho baada ya kocha wake kumtoa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine wakati timu yao iliposhinda dhidi ya Highlanders katika michuano ya kombe la Irn- Bru hatua ya robo fainali.

Liam alitoka moja kwa moja hadi katika benchi na kuanza kumlaumu kocha wake kuwa pamoja na kufunga bao lakini bado alimtoa nje.

Kocha wake alipojaribu kumuelewesha, alianza kumshambulia kwa ngumi za kutosha hadi waliokuwa katika benchi kuingilia na kuamua ugomvi huo.

Kocha Scott Kellacher alilazimika kujilinda kwa kila namna wakati Polworth akimshambulia akiwa katika benchi, kabla ya kumshambulia kocha wake, Polworth alifunga bao la pili na mechi iliisha wakishinda kwa mabao 3-1.

Please follow and like us:

Comments

comments