MBASHA NA SKENDO YA KUTOKA NA MKE WA MTU

• Adaiwa kumpost katika page yake ya Instagram akimtakia heri ya kuzaliwa na kummwagia sifa kibao

Muimbaji wa nyimbo za Injili hapa Bongo Emmanuel Mbasha ambaye alitengana na mkewe Flora anadaiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamke anayesemekana kuwa ni mke wa mtu.
Skendo hiyo imekuja baada ya hivi karibuni baada ya Mbasha kuonekana akiwa close na mwanamke huyo katika picha ya pamoja ndani ya gari hali iliyosababisha watu kusema kuwa amekuwa na mahusiano na mwanamke huyo kwa siri tangu muda mrefu na kuongeza kuwa katika birthday ya mwanamke huyo Mbasha alimpost na kummwagia sifa kibao.
Licha ya hayo yote Mbasha amekuwa akikataa kuwa hana uhusiano na mwanamke huyo na kusema kuwa ni mtu ambaye anaheshimiana naye tofauti na watu wanavyofikiria na kuongeza kuwa Yule dada tayari ana mume wake.
“Tafadhali sana jamani naomba muwe waungwana, huyo dada tunaheshimiana sana na siwezi kufanya kitu chochote kibaya na ukizingatia mumewe pia tunaheshimiana, nawaheshimu sana hao jamani” alisema Mbasha.

Please follow and like us:

Comments

comments