Majukumu ya Tambwe kuchukuliwa na Chirwa

http://1.bp.blogspot.com/-PcQv0Bxa480/VQ52GN53dXI/AAAAAAABfLY/0hRwe0k4nvk/s1600/TAMBWE.jpg

       Kutokana na Tambwe kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha la goti na kumsababishia kukosa mechi tano ambazo Yanga imecheza ikiwepo mchezo wa ngao ya jamii na minne ya ligi kuu Bara Kocha mkuu wa Yanga amemkabidhi Obrey Chirwa majukumu ya Mshambuliaji Amissi Tambwe.

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema kukosekana kwa Tambwe hakuna tatizo lolote kwani Chirwa yupo na atabeba majukumu yote ya Tambwe kwa muda huu ambao mchezaji anauguza goti lake.

“Ninachokifanya ni kwamba, kwenye kikosi changu natengeneza ile hali ya kwamba akikosekana mmoja basi anakuwepo mwingine wa kuziba pengo lake”alisema Lwandamila.

Please follow and like us:

Comments

comments