MAGUFULI NA MUSEVENI WAWEKA UZITO BOMBA LA MAFUTA

• Ni baada ya kutoa maagizo kuwa ujenzi wa bomba hilo ukamilike mapema kabla ya mwaka 2020


Rais John Magufuli ametaka ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ukamilike mapema kabla ya mwaka 2020 ili uzalishaji wa mafuta uanze.
Rais Magufuli ambaye yupo nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu alisema hakuna sababu ya kuchukua muda mrefu kwa sababu mkandarasi anaweza kufanya kazi kwa saa 24, lakini pia kazi hiyo inaweza kugawanywa kwa wakandarasi 10 kila mmoja ajenge kilomita 145.
Kauli hiyo aliitoa jana alipoungana na Rais Yoweri Museveni wa Jamhuri ya Uganda katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi huo. Jiwe hilo liliwekwa kwenye kijiji cha Luzinga, mkoa wa Rakia nchini Uganda baada ya uzinduzi kama huo kufanyika kwanza Chongoleani, mkoani Tanga, Agosti 05, mwaka huu.
“Wataalamu wa Tanzania na Uganda mkae pamoja ili kuhakikisha ujenzi wa bomba hili lenye urefu wa kilomita 1,445 unakamilika kabla ya mwaka 2020. Mnaweza hata kuweka wakandarasi 10 ili kazi iishe hata mwaka 2019,” alieleza Rais Magufuli na kushangiliwa.

Please follow and like us:

Comments

comments