LULU MAHAKAMANI

 

  • Ni katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili

 

 

 

Kesi inayomkabili muigizaji maarufu hapa nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imeanza kusikilizwa leo ambapo Lulu aliwasili mahakamani akiwa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudi aliyekuwa muigizaji mwenzie Steven Kanumba kilichotokea April 7, 2012 nyumbani kwa marehem, Sinza, Vatkan.

Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni hapa nchini, Lulu amesema kuwa yupo tayari kukabiliana na kesi hiyo, ambapo yeye alijua ipo siku itarudi tena huku akieleza kuwa taarifa ya kurudiwa kwa kesi hiyo aliipata kabla watu hawajapata kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa.

“Unajua watu hawajui sheria, kesi haikwahi kuisha ni procedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa, siyo kama imeibuka tu, na kwa sababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kisheria na sio kama nyie kwenye mitandao nap engine nilipata kabla yenu” alisema Lulu.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa, kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla.

Please follow and like us:

Comments

comments