LULU KUKAA GEREZANI MIEZI MITANO

• Mrembo huyo atapaswa kutumikia theluthi ya kifungo chake gerzani kabala ya mchakato wa kukata rufaa kukamilika

Msanii wa fi lamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu alianza kutumikia kifungo cha miaka miwili juzi baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumtia hatiani kwa kumuua bila ya kukusudia msanii Steven Kanumba.
Akitoa ufafanuzi wa kisheria katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Wakili wa Lulu, Peter Kibatala alieleza kuwa hakuna cha kufanya kwa Lulu kabla ya kutumikia theluthi ya kifungo chake. Alisema kisheria katika miezi hiyo mitano ya kutumikia kifungo, wanaweza kuomba dhamana wakati wakisubiria rufaa na kama Lulu atakuwa na bahati anaweza kupata wakati wowote.
Wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole alisema sheria ya makosa ya jinai inasema adhabu ya juu kwa mashitaka ya kuua bila kukusudia ni kifungo cha maisha lakini hakuna ukomo wa adhabu ya chini. Kambole alisema mahakama inaweza kutoa adhabu ndogo kutokana na kigezo cha umri, muda wa kukaa gerezani kwa mshitakiwa na kama ni mkosaji wa kwanza na kajutia kosa.
‘’Mahakama ndiyo inayoamua kutoa adhabu kwa kuwa sheria inaonesha adhabu ya juu ni kifungo cha maisha lakini hakuna ukomo wa adhabu ya chini hivyo inaweza kumhukumu kifungo cha nje, kifungo cha miaka miwili au mmoja kulingana na sababu hizo,’’ alisema Kambole.

Please follow and like us:

Comments

comments