LAMAH ATOA UMUHIMU WA TUNZO NA ALBAMU

 

  • “tunzo ina umuhimu wake kwa sababu unapoipata inakuhamasisha kufanya vizuri  zaidi”

 

 

         Kutoka Fish Crab Records Producer Lamah amezungumzia umuhimu wa wasanii kupata tunzo na wasanii kutoa nyimbo zao kwa mfumo albamu.

Producer huyo amesema kuwa kukosekana kwa tunzo kunapunguza ushindani baina ya wasanii pia msanii anapotoa albamu, ndio kinakuwa kipimo chake katika kujua na kuweka vionjo tofauti tofauti.

“tunzo ina umuhimu wa kukuhamasisha katika kufanya vizuri kazi yako na kukuletea ushindani na wenzako, na tunzo inapokesekana game la muziki linakuwa ni la kawaida sana” alisema Lamah na pia kwa upande wa albamu producer huyo alieleza kuwa

“Albamu pia ina umuhimu wake kwa sababu inakupa kipimo cha wewe msanii kuweza kufanya ladha tofauti kwenye albamu yako, kama utafanya RnB, hip hop, Bongo Flava, Jazz kwa hiyo kwenye albamu utaweka nyimbo nane ambazo zitazokuwa tofauti tofauti, utaondoka utafanya featuring na msani fulani, kwa hiyo albamu ina umuhimu wake”, alisema Lamah.

Please follow and like us:

Comments

comments