KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE 2017

  • Rais kutoshiriki maadhimisho ya baba wa taifa kutokana na majukumu mengine ya kiserikali

 

http://www.bongomovies.com/wp-content/uploads/2016/10/NYEYERERE.jpg 

Baada ya kutangazwa katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika kumbukumbu ya Baba wa Taifa, taarifa imetolewa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya Rais kuwa Magufuli hatakuwa mgeni rasmi katika kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kama ilivyotangazwa.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba tarehe 11 octoba ambayo ndiyo inatangazwa kufanyika kwa kongamano hilo Mheshimiwa Rais atakuwa na majukumu mengine ya kitaifa kulingana na ratiba yake ya kazi na kuwataka watu wote kuzingatia utaratibu.

Hata hivyo wamezitaka taasisi mbalimbali za umma na zisizo za umma zinazomualika Rais katika kumbukumbu ya Mwl.Julius Nyerere zinakumbushwa kutotangaza ushiriki wa Mhe.Rais mpaka zipate uthibitisho kutoka Ofisi ya Rais.

Kila mwaka tarehe 14 Octoba ni kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki dunia tarehe 14 Oktoba 1999 nchini London ambako alikuwa amelazwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Please follow and like us:

Comments

comments