KEISHA: WATU WAACHE UZUSHI

 

  • Adai kuwa anatarajia kurudi kwenye game kwa kishindo lakini sio kwa kiki ya ndoa ya Dogo Janja na Irene uwoya kama watu wanavyodai

Mwanadada kutoka katika Industry ya Bongo Fleva, Khadija Shabani ‘Keisha’ amesema kuwa muda si mferu anatarajia kurudi kwenye game baada ya kimya cha muda mrefu lakini sio kwa kiki ya ndoa ya Dogo Janja.

Keisha amesema hayo baada ya kusambaa picha akiwa katika ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya na watu kudai kuwa ndoa hiyo ni kiki ya wimbo wa Keisha ambao anatarajia kuutoa kitu ambacho Keisha amekana.

“ Ni kweli narudi kwenye muziki lakini ujio wangu hauna uhusiano kwa namna yoyote ile na kusambaa kwa picha za harusi ya Janjaro na Uwoya, mimi ni muislamu safi nisingeweza kukubali kuhusisha mambo matakatifu ya dini na vitu nya kidunia, watu waache kuzusha kuwa ni maandalizi ya video yangu mpya” alisema Keisha.

 

Please follow and like us:

Comments

comments