KAMIKAZE ACHAFUA HALI YA HEWA MTANDAONI

 

  • Ni baada ya kutupia picha ya nusu utupu ya mrembo Feza Kessy

 

         Mwanamuziki anayefanya poa hapa Bongo Cyrill Kamikaze ametoa kali katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kutupia picha ya mwanadada Feza Kessy ambayo inaunyesha mwili wake kwa kiasi kikubwa.

Kamikaze ametupia picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram ambapo pia aliambatanisha na maneno haya chini ya picha hiyo

“nimeshindwa kuvumilia kwa kweli, picha ilikuwa special kwa ajili yangu lakini baby sikuweza kuitunza kwa ajili yangu pekeefeza kessy” ameandika Kamikaze.

Mashabiki wengi wa mastaa hao walionekana kuchefuliwa na picha hiyo na kuanza kumponda Cyrill kwa kudai kuwa amemdhalilisha mrembo huyo.

Hivi karibuni pia mrembo Feza aliingia katika skendo ya kuhusishwa kuwa na mahusiano ya jinsia moja kutokana nay eye kujiita Tom Boy ambapo aliibuka na kusema kuwa kabla watu hawajaanza kupaniki inabidi wajue kwanza maana ya neno hilo ambalo humaanisha mdada anayependelea kujihusisha na shughuli za kiume na kupendelea kuvaa mavazi ya kiume.

Please follow and like us:

Comments

comments