JAY DEE : ASLAY NI MOTO WAKUOTEA MBALI

 

  • Amesema mziki wa aslay unamvutia anaweza kusikiliza hata siku nzima

     Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa ‘I miss you’ Judith Wambura aka Lady Jay Dee amefunguka kukunwa kwake na kazi za msanii mwenzake Aslay Isihaka aka Aslay anazozifanya kwa sasa

     Jide amesema anapohitaji kusikiliza muziki mzuri ,husikiliza nyimbo za Aslay na amekuwa akiusikiliza hata kutwa nzima kwa kuwa kazi zake zinakata kiu ya burudani anayoitaka

“mimi ni mwimbaji ,lakini haina maana kwamba sipati burudani kwa wenzangu ,mfano huwa natumia saa nyingi ,wakati mwingine nashinda kutwa nzima nasikiliza kazi za aslay ,anajua kuimba na kuandika nyimbo nzuri “amesema jaydee

Please follow and like us:

Comments

comments