HUSNA NA MKONGO CHALI

• Pete aliyokuwa amevalishwa kwa sasa imebaki story


Lile penzi la Mmbongo Movie, Husna Maulid na Mkongo Mwami Radjabu imebaki story baada ya Husna kufunguka kuwa kwa sasa hawana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo.
Husna amesema kuwa kwa sasa hana uhusiano wowote na Mkongo huyo na wamebaki kuwa washkaji licha ya kuwa katika mapenzi yao tayari walishafika hatua ya kuvalishana pete.
“ Kwa sasa Mwami amebaki kuwa mshkaji wangu tu na wala sio mpenzi wangu kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Husna.
Kabla ya uhusiano na Husna Mwami ameshawahi kuwa na uhusiano na mastaa wengine wa Bongo kama Jaquline Wolper, Wema Sepetu, Tunda pamoja na Masogange.

Please follow and like us:

Comments

comments