HUDDAH AMMENDEA JUX

 

  • Asema ni mwanaume mwenye muonekano mzuri na anavutia

Mfanya biashara na mwanamitindo maarufu kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe, amesema kwamba anadhani msanii Jux kutoka Bongo ni mwanaume ambaye yeye anaweza kuwa naye katika mahusiano huku akimwaga sifa kuwa ana muonekano mzuri katika mavazi.

Huddah alizungumza hayo wakati akifanya interview na Nirvana baada ya kuulizwa swali iwapo anaweza kuwa katika mahusiano na Mbongo Fleva Jux baada ya kumsifia kuwa ana muonekano tofauti na wenye kuvutia.

 

“Nafikiri ni mwanaume ambaye naweza kuwa naye kwenye mahusiano…… yupo single? Hata mimi nitapatikana….” Alisema Huddah

Hata hivyo Huddah alimashauri Jux kufanya kolabo na wasanii wakubwa zaidi wa kimataifa ili azidi kuwa msanii mkubwa zaidi ndani na nje ya Bongo kwani ana muonekano wa kuwa mtu maarufu.

Huddah alikiri kwamba alishawahi kumchek Jux kupitia mtandao na kumwambia jinsi gani anapenda muonekano wake wa mavazi na jinsi ambavyo anavaa tofauti na jamii zinavyomfikiria.

Please follow and like us:

Comments

comments