HERRY KANE AINYANYUA UINGEREZA

 

  • Ni katika fainali za kuelekea kombe la Dunia

 

Na Audrey Mgalama.

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane ameipa ushindi wa bao moja kwa sifuri (1-0) timu yake ya Uingereza dhidi ya timu Slovenia, goli lililofungwa ndani ya dakika za majeruhi ya 94 na kuifanya timu hiyo kufanikiwa kufuzu kombe la Dunia litakalofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

Katika uwanja wa Wembley, timu ya Uingereza ilihitaji pointi mbili tu ili kupata nafasi ya kushiriki katika michuano hiyo ambapo mataifa mbalimbali duniani yatashiriki.

Timu ya Scotland pia imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Slovakia, ambalo lilifungwa ndani ya dakika za mwisho na Martin Skrtel na kuipa matumaini timu hiyo kwenda kombe la dunia baada ya kuwa katika nafasi ya pili.

 

Please follow and like us:

Comments

comments