HARMONIZE KUPIGA DOUBLE DOUBLE

• Ni baada ya kung’ara na ‘Shulala’ na sasa anatarajia kutoa kichupa kingine na Sarkodie


Neema inazidi kumuangukia Harmoniza ‘Konde boy’ baada ya hivi karibuni kuachia ngoma yake aliyomshirikisha M-Nigeria Korede Bello ‘Shulala’na sasa anatarajia kufanya video nyingine ambayo amemshirikisha mkali wa Hip Hop kutoka Ghana Sarkodie.
Wiki ijayo mmakonde huyo anatarajia kusafiri kwenda kurekodi kichupa kipya na cha ngoma yake aliyomshirikisha Sarkodie na kuongeza kuwa pia tutegemee kazi nyingine aliyoifanya na kundi maarufu la muziki Nchini South Afrika na Afrika kwa ujumla.

Sarkodie

“Wiki ijayo natarajia kusafiri kikazi, nitakuwa nakwenda kufanya video yangu mpya na Sarkodie kutoka Ghana” alisema Harmonize.

Please follow and like us:

Comments

comments