HAMISA APEWA ONYO NA DANUBE

• Ni baada ya kupost video ya tangazo la Danube na kuandika it’s time nije kuchukua hereni zangu

Siku kadhaa zilizopita Hamisa Mobetto alipost video ya tangazo la Danube na kuandika ujumbe uliinyesha kuwa ni kijembe kwenda kwa mpenzi wake Diamond kwani siku za nyuma Zari aliwahi kuzikuta hereni za Hamisa chumbani kwa Diamond.
This time Danube wameamua kumuandikia barua Hamisa wakimtaka aifute video hiyo kwani inaharibu biashara yao na kuchafua jina la kampuni yao na kama hatafanya hivyo basi watamchukulia hatua za kisheria.
Danube wamedai kuwa Hamisa alitumia tangazo lao kwa ajili ya maslahi yake binafsi na kutumia jina la kampuni yao na kuongeza kuwa alipost tangazo hilo katika page yake ya Instagram bila ridhaa yao kitu ambacho ni kinyume na sheria ya kampuni yao.

 

Please follow and like us:

Comments

comments