HAKUNA WA KUNILINGANISHA NA AKINA AMBER LULU

• Adai mkwanja anaolipwa kwenye video queen unamtosha kabisaaa!


Msanii anayekuja kwa kasi hivi sasa, Pretty Kindy amedai kuwa kwa video queen ambao wametimkia katika muziki akiwemo Amber Lulu, hakuna wa kumlinganisha nao.
Pretty amesema kuwa hawezi kukimbia kuwa video queen kama walivyofanya wakina Amber Lulu na Gigy Money na wengine kwa sababu anajiamini na analipwa vizuri na hata kwenye muziki bado hajaona wa kumpa changamoto.
“ Kiukweli hakuna wa kunilinganisha na hao wengine, juzikati nilikula dili la uvideo queen kwenye ngoma ya Benny Kinyaiya na nililipwa vizuri sana, lakini siwezi kuikimbia tasnia hiyo, kisa malipo, maana kama ni fedha ninajua nitalipwa za kutosha” alisema mwana dada huyo.

Please follow and like us:

Comments

comments