CR7 AFIKISHA MECHI 400 MADRID

Hapo jana wakati timu ya Real Madrid ikiivaa Dortmund ya Ujerumani katika ligi ya mabigwa wa ulaya, mchezaji Christian Ronaldo amefanikiwa kuichezea timu hiyo mechi 400 tangu ametua katika timu hiyo akitokea Manchester United na tayari Ronaldo ameichezea timu ya Real Madrid mechi za La Liga 267.
Pamoja na hayo gwiji la Real Madrid Raul Gonzalez ndiye anaeshikilia nafasi ya kwanza kwa kuichezea timu hiyo mechi 741 katika michuano yote, hii ni tangu kuanzishwa kwa Real Madrid ambayo ni moja ya klabu kongwe ulaya na duniani kote ambapo ni wachezaji 22 tu walioweza kufikisha mechi 400.
Baada ya beki Mbrazil, Roberto Carlos aliyefanikiwa kucheza mechi 527 na beki mwingine Mbrazil ambaye bado anacheza, Marcelo aliyefikisha mechi 416, kwa sasa Ronaldo anakuwa mchezaji wa tatu mgeni kucheza mechi nyingi za real Madrid.

Please follow and like us:

Comments

comments