CHIBUDEE ATEMA CHECHE

  • Achoshwa na wanaomuhusisha kuwa kwenye mahusiano na warembo tofautitofauti

 

 

Msanii Chibu Dee au jina la kutafutia ugali Diamond Platnumz ameamua kuvunja ukimya na kutoa ya moyoni kwa wote wanaofuatilia love life yake. Kupitia ukurasa wake wa instagram Mond aliandika hivi,

“Mara Diamond kamla huyu, mara sijui nasikia anatembea na huyu, mara Ooh sijui inasemekana juzi alikuwa na huyu…yaani kila ukiamka limezuka jipya. Utazani yangu ina sukari au nakojoa dhahabu…hebu niacheni kidogo, niko busy nahangaika kuipeleka Bongo Fleva yetu duniani…. sijamkaza yeyote, na sina mahusiano na yeyote anaetajwa, na siku pia nikimaliza mahusiano yangu na aliye South na nikawa na mwingine na ikifikia kuliweka wazi nitaliweka wazi mwenyewe, maana hakuna kitachonizuia… ndio kwanza nna miaka 28, sijaoa na hata nikioa naruhusiwa niwe na wake wanne PERIOD!!” aliandika Diamond.

Tujikumbushe kuwa hivi karibuni Chibu aliingia katika skendo ya kutoka kimapenzi na mrembo Dillish Methew kutoka na nchini Namibia na pia alionekana kuweka matatani mahusiano yake na mrembo Zari The Boss Lady baada ya kukubali kuwa amezaa na mwanamitindo Hamissa Mobetto.

Please follow and like us:

Comments

comments