JUDGE WA MEEK MILL KUCHUNGUZWA NA FBI

• Ni baada ya siku chache kupita tangu alipotoa hukumu ya msanii huyo kufungwa miaka 2 

Ikiwa ni wiki moja tu baada ya Meek Mill kuwekwa jela kwa kosa la violation probation, Judge Genece Brinkley ambaye alihusika katika kutoa hukumu hiyo yupo chi ya uchunguzi na FBI.
Chanzo cha habari kinasema kuwa FBI imekuwa iki-monitor proceedengs za Meek kwa muda sasa na wanafanya uchunguzi kwa Judge Brinkley kama ana matumizi mabaya ya madaraka.
Inasemekana kuwa Judge huyo ana-beef binafsi na rapper huyo kwani aliwahi muomba Meek kumpa shoutout katika wimbo wa “On Bended Knee” lakini Mill alikataa kufanya hivyo.

Please follow and like us:

KYLIE JENNER ACHUKIZWA NA BABY SHOWER YAKE

• Alitamani ifanyike katika club ya Los Angels inayo-trend sana lakini haikuwa hivyo


The last born kutoka katika familia maarufu nchini Marekani ya The Kardashians Kylie Jenner amechukizwa na almost kila kitu katika party yake ya Baby shower.
Mrembo huyo mwenye umri wa mika 20 ambaye anatarajia kupata mtoto with her boyfriend Trivis Scott alilazimika ku-held a boring party nyumbani kwake kama sehemu ya kuendeleza reality show yao ya Keeping Up with the Kardashians.


“ilikuwa ni pajama party katika bustani, marafiki wote walikuwa organized na ma-producer pamoja na mama yake aitwaye Kris. Kris ni producer kwahiyo alikuwa aki-manage episode ya kipindi cha KUWTK. Marafiki wa Kylie hawakuweza kutumi mitandao ndio maana picha hazikuvuja na kila mmoja alizuiwa ku-take selfies kwa ajili ya Snapchat just in case” alisema insider.
Boyfriend wa mrembo huyo pia hakufanikiwa kufika katika party hiyo kutokana na commitments za tour za kimuziki.

Please follow and like us:

MOO DEWJI ATOA SOMO NAMNA YA KUTUMIA MUDA

• Adai kuwa maisha ni mafupi kuutumia muda katika mambo yasiyokuwa na msingi

A former politician ambaye kwa sasa ni mfanya biashara maarufu katika jiji la Dar es Salaam Moammed Dewji ambaye anafahamika sana kwa jina la Moodewji amefunguka maneno ya msingi kuhusiana na matumizi ya wakati.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram tajiri huyo ameandika kuwa,
“Wekeza muda wako kwenye vitu ambavyo vitakusaidia kukua na kuendelea mbele. Maisha ni mafupi sana kujihushisha na maongezi yasiyo na faida” ameandika Moodewji.
Moodewji ni CEO na Rais wa kampuni MeTL Group ambayo ilikuwa ya baba yake hapo mwaka 1970 na pia aliwahi ku-serve katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 2005-2015 for his home town Singida.

Please follow and like us:

THE BEST FEMALE ARTIST OF EAST AFRIKA NI NANDY

• According to Afrima mrembo huyo ndiye aliyejinyakulia tunzo ya kuwa msanii bora wa kike

Mwanadada Nandy aka The African Princess ambaye anafanya poa sana katika industry ya music ikiwa tu ni muda mchache tangu kuingia kwake katika game.
Nandy ambaye kwa sasa anakimbizana ngoma yake ya “wasikudanganye” usiku wa kuamkia leo ameibuka mshindi wa tunzo za AFRIMA na kuwa mwanamuziki bora wa kike kwa mwaka 2017.
Tunzo hizo ulifanyika katika nchi ya Nigeria ambapo mastaa kibao walikuwa nominated katika categories tofautitofauti.
Msanii mwingine kutoka Bongo ni Alikiba aliyeshinda tunzo ya best artist or group in African RnB and soul na pia katika The Best collabo in Africa ngoma ya “Aje” imechukua.

Please follow and like us:

SOUDY BROWN ATEMA CHECHE

• Ni baada ya mrembo mmoja kumlalamikia jamaa huyo kutumia lugha moja tu akiwa anagawa ubuyu

Mwandishi na mtangazaji machachari wa kipindi maarufu hapa town cha Shilawadu Soudy Brown ameibuka na kumwaga maneno heavy kwa mmoja wa shabiki wake.
Kupitia mtandao wa Instagram Soudy ametokwa na maneno hayo baada ya fan huyo kuandika kuwa,
“He! He! He! Soudy, kwahiyo pale ambapo ni matangazo ya biashara in London unaweka caption za kiingereza ili fans wako wa London waweze kukuelewa vizuri lakini ikiwa ni suala la umbeya basi unaweka caption za Kiswahili ili fans wako wa London wasikuelewe, sisi pia tunataka caption za kiingereza katika posts zako za gossip” ameandika fan huyo ambapo Soudy hakusita kuijibu kuwa,
“My dear, hukunilipia ada yangu ya shule, pili, kuandika ubuyu(umbeya) kwa kiingereza haunogi kwahiyo usinichoshe kuandika English, na tatu kiingereza huku kimekuja na Boti” ameandika Soudy.

Please follow and like us:

WIZKID APOTEZA FAHAMU IN A CLUB

• Ni baada ya kudaiwa kutumia madawa ya kulevya kwa kiasi kilichopitiliza

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Wizkid aka Starboy ameripotiwa kuwa hapo jana ali-faint mara baada ya kumaliza show yake nchini Uganda katika mji wa kampala, kwa kuzidisha madawa ya kulevya.
Issue ya madawa ya kulevya kwa wasanii mabalimbali hasa wa nchini Nigeria, imekuwa ikikipeleka kiwanda cha muziki katika level ambayo ni negative.
Ripota mmoja ameeleza kuwa ilikuwa ni jambo la ghafla sana ambapo mara baada ya Wizkid kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya immediate treatment na shughuli katika club hiyo kufungwa.
Inasemekana kuwa majibu yalipotoka yalionyesha kuwa kulikuwa na chembechembe za unidentified drugs.

Please follow and like us:

REKODI YAVUNJWA KATIKA MLIMA MREFU AFRICA

• Ni baada ya raia wa Hispania kufanikiwa kuvunja rekodi yakuupanda mlima huo kwa baiskeli

Mpanda milima mashuhuri duniani kwa kutumia Baiskeli, Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli kwa siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito na wenzake wawili, Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema, aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika
Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa za Kilimanjaro, Arusha na Saadani inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio vya utalii katika Hifadhi zake 16. Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anaeleza hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.

Please follow and like us:

RAIS TRUMP AUKANA UZEE

• Ni baada ya Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kumuita mzee na mchochezi


Wakati vita vya maneno vikiendelea kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un inaonekana Trump kuguswa zaidi na kauli zilizotolewa na serikali ya Korea Kaskazini kwa kumuita kuwa ‘mzee na mchochezi wa vita’ kitu ambacho kimemfanya aweke wazi hisia zake kuwa angefurahi siku moja kuona wanakaa meza moja na Kim.

Wizara ya mashauriano ya nchi za kigeni nchini Korea Kaskazini jana ilimuita Trump kuwa ‘mchochezi wa vita na mzee’ na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya kutengeneza silaha za nyuklia.
Kauli ambayo Rais Donald Trump alishindwa kujizuia kuijibu kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee wakati yeye hata siku moja haijawahi kutokea kumkebehi kuwa mfupi na mnene.

“Kwanini Rais Kim Jong-un ananitukana kuwa mimi ni mzee wakati mimi hata siku moja sijawahi kumuita yeye mfupi na mnene? Sawa najaribu kila niwezalo kuwa rafiki yake najua ipo siku tutakuwa marafiki.“ameandika Rais Donald Trump.

Please follow and like us: