SAKATA LA MADAWA TISHIO BONGO, BAADHI YA MASTAA ZIII! KWENYE BATA

Kufuatia msala wa kutuhumiwa kujihusisha na utumiaji au biashara ya madawa ya kulevya unaosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, sasa baadhi ya mastaa wanadaiwa kukauka kwenye viwanja vya starehe, kwa mujibu wa Risasi hii ni  habari kamili.

Chanzo makini ambacho ni mmoja wa mastaa, alifunguka kuwa tangu sakata la kutajwa majina lilipoanza hali ni mbaya kwa mastaa hasa wa kike kwani waliokuwa wakiwapa fedha za kufanya mbwembwe mjini wengi wanahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa tayari.

“Ukweli hali ni mbaya kwa sisi mastaa ndiyo maana unaona hata zile mbwembwe za mjini hazipo tena, wengi tunahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa au wadhamini wao.

“Wasanii wa kike ndiyo wenye hali mbaya zaidi kwani wale mapedeshee waliokuwa wakiwapa jeuri wamepunguza kuwapa fedha huku wengine wakiwa wameshatajwa majina hali ambayo inaendelea kuzua hofu zaidi,” kilisema chanzo hicho.

Gigy Money

Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, ni kweli hali ni mbaya kwa mastaa na wengi wao wakiwa na hofu kubwa baada ya kuona wenzao au watu wao wa karibu, wametajwa kwani hata wakipigiwa simu zao za mikononi wana hofu kuzipokea au hata wanapofuatwa majumbani mwao husemekana wamesafiri.

Amber Lulu

Uchunguzi huo ulibaini kuwa, kwenye kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar, hivi sasa pamekauka kwani wahudhuriaji ni wachache huku mastaa wakiwa hawaonekani kama ilivyokuwa zamani walipokuwa wakijirusha.

Siyo kwenye viwanja tu, lakini pia hata ngoma mpya zilizoachiwa hivi karibuni hazina msisimko kwenye kumbi hizo kama zamani, mfano ukiwa ni wimbo mpya wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake wa Mary You akimshirikisha mwanamuziki wa Marekani, Ne-Yo.

Gigy Money

Pia siku kadhaa zilizopita wasanii wakali kwenye Bongo Fleva, Diamond, Ali Kiba na Navy Kenzo walipata tuzo zilizotolewa Kampala nchini Uganda zilizojulikana kwa jina la Hapipo Awards, lakini hazikuwa gumzo kama kipindi kingine zinavyokuwa na hii yote ni kutokana na sakata la madawa ya kulevya.

Amber Lulu

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, nako kumepoa kwani ishu kubwa inayojadiliwa ni masuala ya madawa ya kulevya jinsi watu wanavyotajw a , wale mastaa wa liozoea kuposti picha na mambo yao mbalimbali kwa sasa wanaonekana kupoa, jambo ambalo ni tofauti na zamani.

Baadhi mastaa ambao kabla ya ishu ya madawa ya kulevya walikuwa hawakosi klabu lakini sasa hawaonekani ni pamoja na Gigy Money, Amber Lulu, Aunty Lulu, Isabela Mpanda, Shilole, Wema, Uwoya, Baby Madaha na wengine kibao. Akizungumzia ishu hiyo, Amber Lulu alisema:

“Naona maisha yako vilevile, sina wasiwasi kwani wale waliokuwa wanategemea wanaume waliotajwa ndo’ wenye shida.”

Naye Isabela Mpanda alifunguka:

“Ni kweli, hali inazidi kuwa ngumu japokuwa huwa sipendi kwenda klabu kwani mimi ni mwanamuziki na sipendi kuonekana sana ili nisizoeleke.”

Aunty Lulu yeye alisema: “Mimi nilishabadilika hata kabla ya ishu za madawa ya kulevya ila kwa wale waliokuwa wanategemea wanaume wa madawa ya kulevya ndiyo wana hali mbaya na lazima mwaka huu tuheshimiane.”

 

Please follow and like us:

KAMA HAUNA MPENZI HII NI FURSA NZURI KWAKO!

Moja kati ya vitu vizuri ambavyo vinategemea ku-trend East Africa 2017 ni “Hookup” reality show  ambayo inamkutanisha kijana asiye na mpenzi ili aweze kupata mpenzi mwenye sifa ambazo anazihitaji, Tunaamini uzuri wa mwanake bora au mwanume bora sio sura.

Hivyo ukiwa kama kijana utapewa fursa ya kuongea na mtu ambaye haujawahi kumuona utamuuliza maswali kisha utafanya chaguo lako, baada ya kulizika na majibu yake, hiyo inaweza kuwa safari ya kutimiza ndoto yako katika  Mapenzi, #The return of Baabkubwa Magazine 2017 Don’t miss.

        Watch Hookup East Africa Reality Show Episode 1

 

 

Please follow and like us:

NUH MZIWANDA ATACHOROPOKA KWA SHILOLE MSIMU HUU?

Ni miezi kadhaa tangu taarifa zienee za kuyeyuka kwa penzi la Shilole na Nuh Mziwanda, wawili hao wali-trend kinoma kwenye mitandao ya kijamii pia kwenye media mbali mbali za hapa Bongo, haikutosha Nuh Mziwanda ali-hit na wimbo wake wa ‘Jike Shupa’ ambao ulidhaniwa kum-diss Shilole mara baada ya kutengana kwao.

Hazikupia siku nyingi Nuh Mziwanda aliopoa mtoto wa kike na kuamua kumuoa huku Shilole akiwa na misheni town zake!. Siku chache zilizopita Nuh na Silole wameoneka kuanza kurudisha ukaribu wao kwa kupostiana picha pia kufanya show za pamoja kama ilivyo kuwa awali kabla ya kuachana. je watarudiana kimapenzi……?.

Tumeligundua hili baada ya kufuatia acount zao za instagram na kujionea jinsi ambavyo wawili hao wameanza kusapotiana na kujiweka karibu.

Huyu ndio mke wa Nuh Mziwanda

Nuh Mziwanda -“Binadamu haishiwi maneno’kuamua kuoa si jambo dogo Kama wao wanavyofikiria ‘mana wangeshaoa pia ‘ila ni hekima zako ,busara na tabia njema ulitunukiwa na Mungu baba’kuna msemo unasema Maisha popote na una maana kubwa sana kwangu ‘iwe jangwani,vitani,majinj,nitatafuta ridhiki mradi upendeze na kupata shibe wewe na mwanangu inshaalah (NATAFUTA FOR YOU NAWAL).nakupenda sana Mke wangu” .

By  Victor Petro

Please follow and like us:

LADY IN RED 2017 ILIVYO FUNIKA KING SOLOMONI HALL JUMAMOSI

Mambo yalikuwa ni mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall, usiku wa 11/2/2017 lilikuwa ni tukio zito tena lenye furaha na faraja kwa wadau mbalimbali wa mitindo hapaTanzania. Lady In Red 2017 imekuwa ya kipekee zaidi baada ya wadau wengi kuitikia wito. Kwenye hiyo, Fashion Show wabunifu walioshiriki usiku huo walionekana kufanya vizuri zaidi. 

Kwa upande wa Wabunifu ukweli walijipanga na kila mmoja alijaribu kutumia ujuzi wake katika kubuni kazi nzuri, hata wale upcoming Designers, walijitahidi kuandaamavazimazuri kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu kujua nani upcoming na nani nimzoefu katika Tasnia hiyo, hongera yao. Red carpet ili ng’ara na ku-shine zaidi coz watu walijipatia picha nzuri za kumbukumbu, bilakusahau interviews kutoka kwenye media tofauti tofauti za hapa Bongo.

Kumbuka Show hii huandaliwa na Mama wa Mitindo maarufu kama
Asya Idarous Khamsin, akishirikiana na wabunifu wengine. Katika Show hiyo walikuwepo designer wengi + models kama Martin Kadinda,Rukia Walele, Agusta Masaki,Kulwa Mkwandule,  Ally Remtula, JamesMaunda,
PaulinaMgeni, Omary Rashidi, Agness Bwagilo, Kasikana, na wengine kibao.
Hivyo ndivyo mambo yalivyo kuwa Tazama picha za tukio hapa 
by Victor Petro.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Please follow and like us:

WIZ KHALIFA AMCHAPA KISS ZITO AMBER ROSE KWENYE RED CARPET!

Jibril Thomaz, maarufu kama Wiz Khalifa, ambaye ni American rapper, songwriter, and actor, Jumamosi iliyopita amefanya balaa jingine kwenye umati wa red carpet ya pre-Grammy akiwa na mrembo Amber Rose.

Ilikuwa ni siku pendwa kabisa coz it was a weekend 11 Feb, 2017 the former couple nchini Marekani ya Wiz Khalifa and Amber Rose ilionekana kupamba moto baada ya wawili hao kutoka out na kuelekea kwenye  pre-Grammy party iliyo fanyika pale Beverly Hills.

Couple hiyo ili-trend kwenye red carpet baada ya Wiz Khalifa na mpenzi wake kuchapana kiss nzito nzito kwenye umati huo, look at the top photo hivyo ndivyo mambo yalivyo kuwa. Kumbuka Wiz and Amber wana mtoto wa kiume ambaye jina lake ni Sebastian.

By Victor Petro.

 

 

 

 

 

Please follow and like us:

VIDEO: KAULI YA LEMUTUZ KWENYE SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

Moja kati ya mastaa wakubwa kwenye mitando ya kijamii like instagram hapa Bongo ni pamoja na Lemutuz’ hata ukijaribu kutembelea Insta-profile yake utakutana na maelezo haya, 2016 BEST INSTA. AWARDS EDUCATIONAL PAGE – AFRICA SWAHILI RADIO & TV -Permanent Ambassador.

Ok! Baada ya sakata la biashara ya madawa ya kulevya kuendelea kupamba moto katika jiji la Dar es salaam Baabkubwa Magazine tumemnyaka Le Mutuz Nation ili kupata mawazo yake kuhusiana na suala hilo, hapa tumekuwekea video ya Lemutuz akizungumza kuhusu Biashara ya madawa ya Kulevya…..#The return of baabkubwa Magazine 2017 Don’t miss by Victor Petro.

Please follow and like us:

HIKI NDIO ALICHO KIANDIKA WEMA SEPETU BAADA YA KUPATA PIGO ZITO LA MADAWA

Baada ya Mcheza filamu wa kike hapa Bongo ambaye aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kupata pigo zito katika maisha yake, hiki ndicho alicho amua kufunguka kwa Watanzania kupitia Acount yake ya Instagram. #The return of Baabkubwa Magazine 2017 Don’t by Victor Petro.

“Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia. Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu.

Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote. Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge. Asante sana.
Familia ya marehemu Mzee Issac Sepetu”

Please follow and like us: