BANDA AWAPA SOMO SIMBA

 

  • Aliwahi kuwa beki wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga Baroka ya Afrika Kusini

 

Beki kisiki wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda, amesema kama Simba watazubaa na kuamini watatwaa ubingwa kirahisi, watakuwa wanajidanganya na hawataweza kubeba taji la Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kauli hiyo ya Banda imekuja baada ya kuiona timu yake hiyo ya zamani ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi tano mpaka sasa.

Msimu uliopita Banda aliisaidia Simba kuchukua ubingwa wa Kombe la FA na kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara.

Banda aliyekuja kuichezea Taifa Stars dhidi ya Malawi leo katika mechi ya kirafiki, alisema Simba

inatakiwa kusimamia kiwango ilichonacho kwa sasa ili kufikia malengo na si kubweteka kama ilivyokuwa msimu uliopita.

 

 

“Tatizo linaloweza kuwafanya Simba wasitwae kombe msimu huu ni wingi wa mastaa waliowasajili kwani timu ikijaa mastaa mara nyingi suala la kujitoa huwa linapungua na mara kadhaa kujikuta wakiishia kuunda makundi mwaka jana nikiwa Simba tuliongoza kwa pointi nyingi tu, lakini tulishindwa kusimamia msimamo huo kufuatia kuwa na mambo mengi, hivyo kwa mechi hizi tano siwezi kuwapa ubingwa labda wakomae maana bingwa hujulikana mwisho wa ligi,” alisema Banda

Please follow and like us:

Comments

comments