Gumzo Jijini Dar es salaam kuhusu Kuvamiwa kwa Clouds Media

Weekend hii kuamika wiki ya leo jumatatu imezidi ku-trend kwenye social media mbalimbali kufuatia sakata la kuvamiwa kwa kituo cha redio cha Clouds Fm kilichopo Mikocheni Dar es salaam.

Tukio hilo la kuvamiwa kwa kituo hicho ilioneka kupitia Video ambayo ilichukuliwa na kamera za CCTV, ilianza kusambaa mitandaoni siku ya Jumamosi asubuhi na kuzua taharuki kwa wananchi wakitaka kujua ni nini kilitokea mjengoni hapo.

Baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, Clouds Fm wametoa taarifa wakieleza nini kilitokea.

Please follow and like us:

Jay Moe – Nisaidie Kushare (Official Music Video)

Hit maker wa ngoma ya ‘Pesa Madafu’ Jay Moe ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaokubalika kwenye muziki wa Hip Hop Bongo ameachia video ya wimbo wake mpya ambao unaitwa ‘Nisaidie Kushare’ Video imeshutiwa Durban, South Africa , Director Travellah Of KWETU STUDIOS

Please follow and like us:

Professor Jay – Kibabe ( Official Music Video )

Rapper mkongwe kutoka Bongo Tz maarufu kama ‘Professor Jay‘ ambaye pia ni Mhe. bado anaendelea kuwateka mashabiki wake wa muziki hapa ameachia kichupa cha wimbo wake mpya uitwao ‘Kibabe’ itazame video kisha dondosha maoni yako hapo chini Cheers #Kibabe Baabkubwa Magazine kitaani kwako soon.

Please follow and like us:

Mwakyembe apiga marufuku kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku watu kufunga ndoa ya aina yeyote,iwe ya serikali, kimila au ya dini bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.

Amesema hayo Alhamisi hii akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.

Pamoja na mambo mengine, Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na Vifo (RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema kuwa bila kuwa na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.

“Wenzetu nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko nyuma, kwa mfano Mkoa wa Morogoro kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,” amesema.

Please follow and like us:

Chid Banz akutana na Nash Mc baada ya miaka mingi kupita!

Milima haikutani lakini binadamu tunakutana, katika pitapita za huku na kule tumekutana na post ya Nash Mc kwenye acount yake ya Facebook ambapo ameweka picha ya pamoja na  msanii Chid Benz ambaye ni kitambo sana alikuwa hajamtia machoni, katika post hiyo Nash Mc aliyaandika haya……

“Dakika kadhaa zilizopita rafiki yangu wa siku nyingi kabla hatujakua na nafasi kubwa katika Sanaa leo tumekutana studio Kiri Records baada ya miaka kibao. Nilikua nasikiliza hatua za mwisho za wimbo wangu wa Shujaa mara Chuma huyo akaingia,tukacheka saaaaaaaaana.

Nimefurahi sana kukutana na Rashid Abdallah Makwiru Au Chidy Benz sina mengi sana ya Kuongea kwani dah! Amekuja kumpokea Shujaa huku huku studio hakutaka kusubiri.

Please follow and like us:

Jose Chameleone amechia ngoma mpya – “Sili Mujjawo”

Msanii Jose Chameleone kutoka Uganda, ameachia ngoma  mpya inaitwa “Sili Mujjawo”, huku akiwa na majonzi ya kumbukumbu ya kifo cha mdogo wake Emmanuel – AK47, kupitia ukurasa wake wa Instagram Chameleone amepost picha hii na kuitolea maelezo. 

Sikiliza ngoma mpya ya Jose Chameleone hapa chini….

 

Please follow and like us: