Audio: Remix mpya kutoka kwa Wiz Khalifa – Closer

Ni wakati wako wa kuburudika na ngoma mpya kutoka kwa wasanii wa muziki Duniani kote, hapa leo tumekuletea mdundo mwingine mkali kutoka kwa Rapper Wiz Khalifa ambaye ameachia Rimix ya wimbo wa The Chainsmokers’  ‘Closer’.

Enjoy good music from here……

Please follow and like us:

Selekta Davizo-‘Hustle Hard’ (official Music Video)

Some time inabidi uburudike na ku-refresh akili yako kwa kusikiliza ngoma mpya, hapa chini tumekuwekea Dancehall video mpya kutoka kwa  Dj Davizo wa Arusha -Tanzania wimbo unaitwa ‘Hustle Hard’ produced by Jettyman.

                                                     Enjoy From here

Please follow and like us:

JPM amtaka Makonda aendelee kuchapa kazi

 

Rais John Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuendelea kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwasababu yeye ndiyo Rais wa nchi hii.

Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiyo mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.

Mkuu huyo wa nchi amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo badala ya kupoteza muda kufuatilia udaku kwenye mitanfandao.

“Mimi ni rais ninayejiamini, sipangiwi mambo ya kufanya. Hata fomu ya kugombea nilikwenda kuichukua peke yangu, kwa hiyo Makonda wewe chapa kazi,” amesema Rais Magufuli.

Mwananchi.co.tz

Please follow and like us:

Vita ya maneno Donald Trump, Snoop Dogg & Bow Wow!

Kwa mujibu wa taarifa kutoka American basic cable and satellite news television maarufu kama ‘Fox News Channel’  zinasema kuwa vita ya maneno kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump, Snoop Dogg & Bow Wow inazidi kupamba moto.

KupitiaTalk Show maarfu kama ‘The  Five’ iliyopo nchini marekani, co-host Greg Gutfeld amechambua zaidi ….

 

Please follow and like us:

Arsenal yaichapa Tottenham 10-0 na kuingia robo fainali!

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Uingereza upande wa wawanawake Kina dada wa Arsenal waliwalaza wapinzani wao Tottenham 10-0 na kufika robo fainali Jumapili.

Danielle van de Donk alifungia wenyeji hao mabao matatu, naye mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Beth Mead akafunga bao pia mechi yake ya kwanza kuchezea Arsenal.

Chelsea, ambao walishindwa na Arsenal fainali mwaka jana, pia walipata ushindi mkubwa, kwa kulaza Doncaster 7-0. Bristol City walilaza Millwall 5-0.

Liverpool, Notts County, Birmingham na Sunderland pia walishinda kwenye mechi hizo za raundi ya tano. Droo ya robofainali itafanyika baadaye Jumatatu.

Matokeo kamili mechi za raundi ya tano

  • Manchester City 1-0 Reading (Jumamosi)
  • Arsenal 10-0 Tottenham
  • Birmingham 2-0 West Brom
  • Bristol City 5-0 Millwall
  • Chelsea 7-0 Doncaster
  • Liverpool 2-1 (AET) Everton
  • Notts County 3-2 Yeovil
  • Sunderland 3-2 Aston Villa
Please follow and like us:

Sekta ya Nyama matatani nchini Brazil

Rais wa Brazil, Michel Temer, amezihakikishia nchi za kigeni kuwa , kashfa iliyokumba sekta ya Nyama chini mwake, haina maana kuwa bidhaa zake si salama.

Rais Temer amewaambia mabalozi kuwa nchi yake bado imeendelea kuzalisha nyama yenye ubora, ingawa kumekuwa na shutuma kuwa viwanda vyake vikubwa vitatu vimekuwa vikiuza nyama iliyooza kwa miaka mingi.

Serikali ya Brazil ina wasiwasi kuwa Marekani, China na nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kupiga marufuku kuingiza nyama kutoka Brazil baada ya shutuma hizo za kushtua zilizojitokeza siku ya Ijumaa.

Polisi nchini humo walifanya ukaguzi nchi nzima na kushutumu makampuni ya ufungaji nyama JBS, BRF na makapuni mengine madogo madogo kwa kuuza nyama isiyo salama, kuku na bidhaa nyingine za nyama.

Zaidi ya wafanyakazi 30 wa serikali waliokuwa na jukumu la kukagua vitendo hivyo wanachunguzwa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Please follow and like us:

Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2016/17

Tukiangazia kwenye ligi ya EPL  2016/17 yaani English Professional League hapa tumekuwekea jedwali la msimamo wa ligi hiyo.

Nambari Klabu Mechi Mabao Alama
1 Chelsea 28 38 69
2 Tottenham 28 34 59
3 Man City 28 24 57
4 Liverpool 29 25 56
5 Man Utd 27 19 52
6 Arsenal 27 22 50
7 Everton 29 21 50
8 West Brom 29 1 43
9 Stoke 29 -9 36
10 Southampton 27 -3 33
11 Bournemouth 29 -12 33
12 West Ham 29 -12 33
13 Burnley 29 -11 32
14 Watford 28 -15 31
15 Leicester 28 -14 30
16 Crystal Palace 28 -10 28
17 Swansea 29 -27 27
18 Hull 29 -32 24
19 Middlesbrough 28 -13 22
20 Sunderland 28 -26 20
Please follow and like us:

Mengi afunguka haya kuhusu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuvamia Clouds media

Kulia ni mkurugenzi wa IPP Media Reginald Mengi (kushoto) ni Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mh Nape Nnauye, akiwa pembeni na C.E.O wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, katikati ni mkurugenzi wa Habari maelezo Hassan Abbas.

Sakata la kuvamiwa kwa kituo cha Radio cha Clouds FM ndio habari ya jiji kwa sasa. Kufuatia tukio la kipekee ambalo halikuwahi kujitokeza, kwenye media hiyo,  tukio hili limekuwa na uzito kiasi cha kuzua mijadala mbalimbali ya sinto fahamu kutoka kwa Watanzania.

Kwa uzito wa tukio hilo baadhi ya viongozi wa serikali na wamiliki wa vyombo vya habari wamejitokeza na kupinga kilichofanywa na mkuu wa mkoa huyo.

Akiongelea suala hilo katika ofisi za Clouds Media mkurugenzi wa IPP Media alisema kuwa “Mimi nina imani kwamba tuna Raisi anayetupenda sana na tuna waziri anayetupenda sana . lakini mapenzi hayo lazima yaonyeshwe kwa vitendo.

Jambo lililofanyika ni la hatari sana lazima tujiulize mtu huyu (Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam) anapata wapi ujasiri huu? kama alikuwa na bunduki hapa anaweza kwenda nazo popote na pengine kuna siku atazitumia”. # Reginald Mengi.”

Please follow and like us: