KISWAHILI KUWA LUGHA RASMI AFRIKA MASHARIKI.

 

 

http://apjcn.nhri.org.tw/SERVER/Africa/swifs/East%20Africa_map_web%20site%20content.JPG

Uongozi wa afrika mashariki (EAC) umesema una mpango wa kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa rasmi katika jumuiya hiyo yenye zaidi ya watu milioni 150.

Liberat Mfumekeko ambaye ni katibu mkuu wa EAC amesema hayo alipokuwa akiongea na balozi mpya Richard Kabonero wa Uganda nchini Tanzania kwenye ofisi za makao makuu jijini Arusha.

Wakati wa hafla ya kufungwa kwa mkutano wa kwanza wa kimataifa ulioandaliwa na Tume ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (EAKC), Naibu waziri mkuu wa Uganda anayeshughulikia masuala ya EAC Kirunda Kivejinja alisisitiza umuhimu wa wananchi kwenye nchi wanachama kukitumia Kiswahili kwa lengo la kuwaunganisha. Kiongozi huyo mbaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri EAC alisema nchi wanachama wa jumuiya hiyo hawatafanikiwa kukitekeleza kifungu cha 137 (2) cha makubaliano ya kuanzishwa jumuiya hio kama hawatakitumia Kiswahili kuwaunganisha.

Wajumbe walieleza umuhimu wa kuanzishwa haraka mabaraza ya Kiswahili na vyama vya lugha hiyo kwenye kila nchi, kutumia lugha hiyo kwenye ngazi mbalimbali za elimu, kuhamasisha tafiti za Kiswahili na nchi wanachama kuitumia lugha hiyo kwenye programu za elimu ya watu wazima.

Please follow and like us: