RAIS TRUMP AUKANA UZEE

• Ni baada ya Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kumuita mzee na mchochezi


Wakati vita vya maneno vikiendelea kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un inaonekana Trump kuguswa zaidi na kauli zilizotolewa na serikali ya Korea Kaskazini kwa kumuita kuwa ‘mzee na mchochezi wa vita’ kitu ambacho kimemfanya aweke wazi hisia zake kuwa angefurahi siku moja kuona wanakaa meza moja na Kim.

Wizara ya mashauriano ya nchi za kigeni nchini Korea Kaskazini jana ilimuita Trump kuwa ‘mchochezi wa vita na mzee’ na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya kutengeneza silaha za nyuklia.
Kauli ambayo Rais Donald Trump alishindwa kujizuia kuijibu kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee wakati yeye hata siku moja haijawahi kutokea kumkebehi kuwa mfupi na mnene.

“Kwanini Rais Kim Jong-un ananitukana kuwa mimi ni mzee wakati mimi hata siku moja sijawahi kumuita yeye mfupi na mnene? Sawa najaribu kila niwezalo kuwa rafiki yake najua ipo siku tutakuwa marafiki.“ameandika Rais Donald Trump.

Please follow and like us:

RAYVANNY AMNYAKUA KIBABE PRODUCER RASHDONI

• Utata ulikuja baada ya Producer Rashdoni kusepa Kiri Records na kwenda Surprise Rocords inayomilikiwa na Rayvann


Producer Rashdoni


Producer maarufu aliyekuwa Kiri Records, Rashdoni amedaiwa kuondoka kimya kimya katika studio aliyokuwa akifanyia kazi hapo awali na kuhamia katika studio za msanii kutoka katika label ya WCB Rayvanny iitwayo ‘Surprise Music Studio’.
Producer anayeshikilia mikoba ya Rashdoni kwa sasa Beya amesema kuwa Rashdoni aliondoka bila kuaga na walikuja kusikia baadae kuwa amehamia katika studio za Rayvanny.
“ Mimi ndio nilikuwa msaidizi wa Rashdoni, Meneja yupo, Bosi yupo lakini aliondoka bila kuaga yaani ilifikia kipindi alikuwa haji kabisa studio au akija ana dash yaani leo anakuja kesho haji, tunakuja kusikia wakati Diamond anafanya interview ya wimbo wake wa fire aliofanya na Tiwa Savage, tukasikia anasema kwamba Rashdoni ndio official producer wa Rayvanny, kwa hiyo sis hatukuwa na la kusema”. Amesema Beya.

Producer Beya

Rashdoni naye alikana tuhuma za kuwa aliondoka bila kuaga na kudai kuwa mkataba wake katika studio hizo ulikuwa umeisha na bosi wake alikuwa analijua hilo.
“ Ukisema kuwa niliondoka bila kuaga unakuwa unakosea, mimi sijawahi kupotea ghafla na bosi aliniuliza nina mpango gani kwa sababu makataba wangu ulikuwa unaisha, nikamwambia bosi tulia nitakuambia nina mpango gani kwa hiyo ofcourse sikumkimbia mtu” alisema Rashdoni

Please follow and like us:

LAMAR: ANAYESEMA MUZIKI HAUNA UTAMBULISHO HATHAMINI CHA NYUMBANI

• Adai kuwa kila mwanamuziki ana identity yake

Producer kutoka katika studio za Fish Crab, Lamar amesema si sawa kusema muziki wa Bongo hauna utambulisho kwani kila msanii ana kitu chake ambacho kinamtambulisha katika kazi zake.

Lamar amewatolea mfano Diamond na Alikiba kuwa wana identity zao ambazo zinawatambulisha katika muziki ambao wanaufanya lakini pia na wasanii wote wa Hip Hop, Bongo Flava wote wana utambulisho wao na unajua kabisa huu muziki umetoka Bongo.
“Kwanza huyo anayesema muziki hauna utambulisho hathamini cha nyumbani kwa sababu muziki wetu una utambulisho, unajua kila muziki una utambulisho wake ila unajaribu kuchukua vitu fulani kutoka sehemu fulani kuleta ladha tofauti, so ukisema muziki wetu hauna utambulisho unakosea sana” amesema Lamar.

Please follow and like us:

BASI LINALOJIENDESHA BILA DEREVA LAPATA AJALI

• Ni katika siku yake ya kwanza tu ya kutoa huduma kwa baadhi ya wananchi


Huko United States of America katika mji wa Las Vegas basi moja linalojiendesha lenyewe bila driver limepata ajali katika siku yake ya kwanza.
Ripoti zinasema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba abiria kadhaa ambapo hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo iliyosababishwa na dereva mmoja wa lori.
Basi hilo lina uwezo wa kuwabeba watu 15 na lina kasi ya kilomita 45 kwa saa lakini kawaida mwendo wake ni kilomita 25 kwa lisaa limoja.
“Basi likafanya kile linastahili kufanya na kusimama. Kwa bahati mbaya dereva wa lori hakusimama, alisema afisa wa mawasiliano Jace Radke.
Ajali za magari yanayojiendesha zimeripotwa awali, lakini karibu ajali hizo zote zimesababishwa na makosa ya wanadamu.

Please follow and like us:

MAGUFULI NA MUSEVENI WAWEKA UZITO BOMBA LA MAFUTA

• Ni baada ya kutoa maagizo kuwa ujenzi wa bomba hilo ukamilike mapema kabla ya mwaka 2020


Rais John Magufuli ametaka ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ukamilike mapema kabla ya mwaka 2020 ili uzalishaji wa mafuta uanze.
Rais Magufuli ambaye yupo nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu alisema hakuna sababu ya kuchukua muda mrefu kwa sababu mkandarasi anaweza kufanya kazi kwa saa 24, lakini pia kazi hiyo inaweza kugawanywa kwa wakandarasi 10 kila mmoja ajenge kilomita 145.
Kauli hiyo aliitoa jana alipoungana na Rais Yoweri Museveni wa Jamhuri ya Uganda katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi huo. Jiwe hilo liliwekwa kwenye kijiji cha Luzinga, mkoa wa Rakia nchini Uganda baada ya uzinduzi kama huo kufanyika kwanza Chongoleani, mkoani Tanga, Agosti 05, mwaka huu.
“Wataalamu wa Tanzania na Uganda mkae pamoja ili kuhakikisha ujenzi wa bomba hili lenye urefu wa kilomita 1,445 unakamilika kabla ya mwaka 2020. Mnaweza hata kuweka wakandarasi 10 ili kazi iishe hata mwaka 2019,” alieleza Rais Magufuli na kushangiliwa.

Please follow and like us:

BOB RISKY FINALLY ADMITS KUWA NI GAY

• Ni baada ya kuonekana kuchoshwa na watu wanaomvamia kwa matusi katika mitandao ya kijamii

Internet personality ambaye pia ni mjasiriamali Okuneye Idris Olarenwaju aka Bobrisky hatimaye amekiri kuwa yeye ni shoga na kuongeza kuwa ataenda tu motoni kwa hilo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bobrisky amefunguka vya kutosha na kuwaponda wale wote wanaomrushia lugha za matusi katika page yake, ambapo aliandika kuwa,
“Wadada wote na wakaka wanaokuja ku-drop comments katika page yangu wote ni wajinga, mnadhani kuwa comments zenu zenye chuki zinaweza kunibadilisha? Mnajaribu sana ku-get my attention, fu*k off my page na mkatafute cha maana katika maisha yenu, yes mimi ni gay, nitakwenda katika moto wa kuzimu, ahsante. Nimechoshwa na maneno yenu nataka kusikiliza something new”, ameandika Bobrisky.BOB RISKY FINALLY ADMITS KUWA NI GAY

Please follow and like us:

KESI YA MOBETO NA MONDI KIAMA

• Leo ndio itafahamika kuhusiana na matunzo yamoto wa Mobetto aliyezaa na Chibu Dee


Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya kesi inayomkabili Diamond Platnumz kuhusiana na matunzo ya mtoto iliyofunguliwa na mwanamitindo Hamisa.
Devotha Kisoka ambaye ni Hakumu Mkazi wa Mahakama hiyo kwa upande wa watoto ndiye anayetarajia kutoa uamuzi huo.
Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kusikiliza hoja kutoka katika pande zote mbili ambapo msanii Diamond alipinga kwa madai kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho sio sahihi.

Please follow and like us:

ODINGA AITUPIA LAWAMA MAREKANI

• Asema kuwa juhudi za wajumbe wao hazijafanikiwa kuzima mgogoro bali wamechangia katika mgogoro wa Kenya


Kiongozi wa Muungano wa NASA, Raila Odinga amewaombwa washirika wa maendeleo wa Kimataifa wa Kenya kujihusisha kikamilifu kusaidia kumaliza mkwamo wa kisiasa nchini humo.
Katika hotuba yake ya dakika 30 akiwa jijini Washington DC, Marekani, Odinga amezitaka nchi za Magharibi kuchukua hatua akisema Wanadiplomasia wa nchi hizo wamejikita zaidi katika kukabiliana na kukua kwa siasa kali na ughaidi huku wakipuuza ufinyu wa demokrasia katika mgogoro juu ya uchaguzi mwaka huu.
“ Nimekuja huku Washington kuwaletea ujumbe rahisi, tunahitaji mshiriki kwa nguvu na kutumia mikono mingi iliyonayo Serikali yenu ili kuwasaidia wajumbe wenu waliopo Nairobi” alisema Odinga katika kituo cha Usalama na Mafunzo ya Kimataifa.
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa “ Serikali ya Jubilee imepora mamlaka ya kila Taasisi ili kufanikisha lengo la kulidhibiti Taifa au walivyojitangazia kutawala hadi mwaka 2032 na Kenya inahitaji uchaguzi mpya na wa kuaminika”.

Please follow and like us: